Klabu ya Sunderland imekamilisha usajili wa mlinda mlango kutoka nchini Ureno Michael Simoes Domingues “Mika” akitokea Boavista.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25, amesajiliwa na Paka Weusi nje ya muda wa usajili kwa huruma ya shirikisho la soka duniani FIFA, ambalo tayari lilikua limeshafunga dirisha la usajili wa majira ya kiangazi mwishoni mwa mwezi uliopita.

Uongozi wa Sunderland uliwasilisha maombi FIFA ya kumsajili Mika ambaye anatokea moja kwa moja katika klabu ya Boavista, kufuatia mtihani uliokua unawakabili wa kuumia kwa mlinda mlango wao chaguo la kwanza Vito Mannone.

Kanuni za ligi ya nchini England zimekua zikivibana vilabu vya ligi kuu na ligi daraja la kwanza kufanya usajili wa wachezaji wenye mikataba na klabu zao mara baada ya dirisha la usajili kufungwa, lakini kanuni hiyo imelegezwa kwa wachezaji ambao wapo huru kusajiliwa wakati wowote wa msimu.

Mika, amewahi kuitumikia timu za taifa za vijana za Ureno chini ya umri wa miaka 20 na 21, na alijiunga na klabu ya Boavista misimu miwiwli iliyopita. Pia amewahi kuzitumikia klabu za Benfica na Atletico CP.

Eddie Howe: Sio Wakati Sahihi Wa Kufikiria Ajira Ya Arsenal
Crystal Palace Wamnasa Mathieu Flamini