Meneja wa kiungo wa Simba, Ibrahim Ajib amesema mchezaji wake huyo, alimndanganya wakala wake aliye nchini Afrika Kusini kuwa mkataba wake na klabu hiyo umekwisha.

Juma Ndambile ambaye sasa yuko Durban nchini Afrika Kusini akiwa na Ajib, amesema mchezaji huyo, mwanzo hakuwa mkweli.

“Unajua wakala alidhani Ajib amemaliza mkataba na Simba, lakini nikamueleza bado mkataba wake upo. Alimndanganya kwa kweli, hakusema ukweli.

“Lakini tayari nimezungumza na wakala wake, maana asili yake ni Tanzania. Tayari ameelewa kwamba Ajib ana mkataba na Simba,” alisema.

Kwa mujibu wa Ndambile, Ajib anatarajia kuanza majaribio leo katika klabu ya Golden Arrows inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.

Mahakama yaamuru Tigo kuwalipa AY, FA mabilioni kwa kutumia nyimbo zao bila idhini
Hamisi Kilomoni: Viongozi Wa Simba Wamejaa Ubinafsi

Comments

comments