Idris Sultan amepata dili ya kuwa balozi wa kampuni ya Uber Tanzania, inayojihusisha na mtandao unaowezesha kuwakutanisha madereva binafsi na wanaohitaji huduma ya usafiri.

Akimtangaza rasmi Idris, meneja wa kampuni hiyo Afrika Mashariki, Elizaberth Njeri amesema kuwa uamuzi wa kumpa ubalozi Idris ni matokeo ya utafiti wa kina uliofanywa na kampuni hiyo.

“Tuna imani kuwa Idris atailetea Uber tija kubwa kwa sababu yeye anawasiliana na mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii kila wakati,” alisema Njeri na kuongeza kuwa muigizaji huyo ana heshima kubwa katika tasnia ya uigizaji na utangazaji.

Naye Idris aliishukuru kampuni hiyo kwa kumpa heshima hiyo ambayo amesema kwake hailengi tu kuwa amepata fedha bali inalenga katika kuwakomboa zaidi vijana wenzake dhidi ya changamoto ya ajira.

Ameitaka Uber kutochukuliwa tu kama program ya kutoa huduma ya usafiri nchini, bali ipewe uzito kama program ya kutoa ajira zaidi.

Idirs amekuwa msanii wa pili mkubwa kuitangaza kampuni ya Uber. Diamond Platnumz pia amewahi kuhusika katika moja ya matangazo ya huduma hiyo.

 

Manchester United yatinga fainali ya kombe la FA
Kigogo CAF apata dhamana, ufisadi wamuandama

Comments

comments