Magwiji wa soka mjini Milan nchini Italia AC Milan, wanajipanga kutuma ofa kaskazini mwa jijini London kwa lengo la kumsajili kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere.

Gazeti la The Daily Star limeeleza kuwa, mpango huo wa AC Milan unasukwa kwa makusudi kufuatia tetesi zinazoendelea baina ya uongozi wa Arsenal na kiungo huyo anaecheza kwa mkopo Bournemouth tangu mwanzoni mwa msimu huu.

Inaelezwa kuwa Wilshere yupo tayari kuondoka moja kwa moja kaskazini mwa jijini London, baada ya kuona hana nafasi katika kikosi cha kwanza, na angependa kucheza kwenye klabu ambayo ina ina ya ushindani wa kweli.

Kufuatia tetesi hizo, AC Milan wanaamini Wilshere atakua na nafasi kubwa ya kupendezwa mkakati wao wa kiushindani katika ligi ya nchini Italia, huku akisaliwa na mkataba wa mwaka mmoja dhidi ya Arsenal.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, amekua akionyesha uwezo mkubwa wa kucheza soka akiwa na klabu ya Bournemouth, jambo ambalo lilisababisha aitwe kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England iliyopambana na Scotland pamoja na Hispania mwezi huu, lakini hakufanikiwa kucheza.

Tayari mchezaji mwenzake kutoka England Joe Hart ameshaanza maisha nchini Italia akicheza kwenye klabu ya Torino kwa mkopo, hivyo inasadikiwa huenda akaingia ushawishi wa kumfuata mlinda mlango huyo, ambaye alionekana hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha Manchester City.

Jurgen Klinsmann Afungasha Virago
Justin Bieber apiga mazoezi na Neymar, atulia na Messi, Suarez