Kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere amesema hatoshangazwa na mashabiki wa soka nchini England endapo watafikia hatua ya kuwazomea wachezaji waliokua wanaunda kikosi cha nchi hiyo wakati wa fainali za Euro 2016, zilizofanyika nchini Ufaransa na Ureno kutawazwa kuwa mabingwa.

Wilshere, amesema anatarajia suala hilo kujitokeza wakati wa ligi ya nchini England, ambayo itaanza mwishoni mwa juma hili kwa michezo kumi kuchezwa katika viwanja tofauti.

Wilshere was part of England's miserable campaign at Euro 2016Jack Wilshere akishuka kwenye ndege, akitokea nchini Ufaransa sambamba na kikosi cha England kilichoshindwa kufurukuta mbele ya Iceland.

Amesema kama itakua hivyo, mashabaki watakua na haki ya kuzomea kutokana na timu ya taifa ya England kufanya vibaya katika fainali za Euro 2016, tofauti na ilivyokua inatarajiwa na walio wengi.

Amesema anaamini mashabiki wengi wanataka kutumia nafasi ya kuonyesha hasira zao kwa wachezaji wa England, wakati wa michuiano ya ligi ya nchi England baada ya kukaa kimya tangu waliporejea wakitokea nchini Ufaransa, siku moja baada ya kufungwa na Iceland mabao mawili kwa moja katika mchezo wa hatua ya mtoano.

Wilshere came on as a substitute in the humiliating defeat by Iceland in the last 16Jack Wilshere akiwa katika hali ya simanzi baada ya mchezo wa England na Iceland kumalizika

Wilshere, mwenye umri wa miaka 24, alikua mmoja wa wachezaji waliokua wanaunda kikosi cha England chini ya utawala wa aliyekua kocha Roy Hodgson ambaye alitangaza kujizulu dakika chache baada ya kufungwa Iceland.

Adnan Januzaj Achukizwa Na Falsafa Za Mourinho
Rio Olimpiki 2016: Ashindwa Na Uzito Wa Chuma Akimbizwa Hospitali