Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Ubelgiji, Adnan Januzaj ameonyesha kuchoshwa mapema na falsafa za meneja mpya wa Man Utd Jose Mourinho.

Habari zilizotolewa na mtu wa karibu na Januzaj mwenye umri wa miaka 21, zimesema kinda huyo haoni matarajio yake katika kikosi cha Man Utd tangu alipowasili Mourinho, jambo ambalo anaona ni sawa na kudhalilishwa.

Taarifa hizo zimesisitiza kuwa suala la Januzaj kutakiwa kufanya mazoezi na kikosi cha vijana cha klabu hiyo, halioni kama ni msaada wa kuendelea kusaidia kukuzwa kwa kipaji chake ambacho tayari kilishawahi kuonekana akiwa na kikosi cha kwanza wakati wa utawala wa meneja David Moyes na kasha Laouis Van Gaal.

Pamoja na hali hiyo bado chanzo hicho cha habari kimeeleza kuwa Januzaj ameonyesha kufurahishwa na taarifa za kuwa sehemu ya mipango ya kutaka kusajiliwa na klabu ya Sunderland ambayo ipo mikononi mwa aliyewahi kuwa bosi wake huko Old Trafford, David Moyes.

Januzaj amekua akitajwa kuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao huenda wakaondoka klabuni hapo katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, kwa kuuzwa moja kwa moja ama kutolewa kwa mkopo, kutokana na kutokukubaliwa kwenye mipango ya Jose Mourinho.

FA Yapanga Ratiba Ya Mzunguuko Wa Pili Wa EFL Cup
Jack Wilshere: Mashabiki Watakua Na Haki Ya Kutuzomea