Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI. Selemani Jafo amewataka Maafisa Utumishi wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuongeza ari ya watumishi wa umma katika kutoa huduma zenye ubora kwa wananchi.

Ameyasema hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha Siku mbili kilichowahusisha Wakurugenzi wa Rasilimali watu wa Wizara zote, Idara zinazojitegemea na Maafisa Utumishi wa Halmashauri zote hapa nchini hii leo mjini Dodoma, ambapo amesema kuwa ni dhamira ya Serikali kuona changamoto za Watumishi wa Umma zinatatuliwa kwa wakati.

“Maafisa Utumishi mnalo jukumu kubwa la kuwasaidia watumishi katika maeneo yao kwa kufanya kazi zenu kwa kuzingatia weledi, kuepuka rushwa, vitendo vya upendeleo na mambo yote yanayoweza kuchafua taswira ya Serikali kupitia huduma mnazotoa,” Amesema Jafo

Amesema kuwa wajibu wa Maafisa Utumishi ni kuwa Kiungo kati ya Wakurugenzi na watendaji wa Taasisi  hali itakayosaidia kupunguza au kuondoa malalamiko yanayofikishwa Ofisi ya Rais TAMISEMI.

.Hata hivyo, Kwa upande Wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Musa Iyombe amewataka Maafisa Utumishi wote kufanya kazi kwa kuzingatia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inalenga kuleta mabadiliko kwa wananchi kwa kuwapa huduma bora.

 

Kagera Sugar yaambulia sare nyumbani
Rais mstaafu atengua kauli

Comments

comments