Asasi za Kiraia (AZAKI) zimetakiwa kutangaza kwa umma shughuli mbalimbali za maendeleo zilizofanywa kwa mafanikio na Serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.

Wito huo umetolewa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo wakati akifunga kongamano la wiki ya AZAKI jijini Dodoma hii leo Novemba 8, 2019.

Amesema ni vyema asasi hizo zikatangaza mambo mema yenye ukweli ndani yake badala ya kutangaza mabaya wanayoyasikia bila kujua ukweli uliopo kitu ambacho ni upotishaji kwa jamii na kinachoweza kuleta taharuki.

“Kuna baadhi ya wanaojaribu kupotosha ukweli sasa kwakua nyie ni watu wa kuleta chachu ya maendeleo basi tangazeni jitihada za maendeleo zinazofanywa na serikali ambazo zimekuwa zikionekana wazi kabisa ” amesema Jafo.

Aidha ameongeza kuwa shughuli za maendeleo yanayotekelezwa yametokana na mchango wa AZAKI baada ya kuibua changamoto zilizopo katika sekta mbalimbali hapa nchini hivyo wanatakiwa kujivunia katika hilo kwa kutangaza matokeo chanya.

Kuhusu utoaji vibali, Jafo amemuagiza Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuhakikisha anasimamia utoaji wa vibali vya usajili wa asasi hizo ili.ziendelew na harakati za kuwahudumia wananchi na kuibua mijadala ya kimaendeleo yenye tija kwa Taifa.

“Sitegemei kusikia malalamiko yeyote kuhusiana na kukwama kwa vibali vya usajili asasi hizi zipewe vibali ili mradi tu vina sera na muongozo inayohitajika ndani ya serikali na zinatekeleza majuku yao kwa mujibu wa miongozo ya kisheria,” amesisitiza Jafo.

Awali Katibu wa NEC itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema AZAKI na Serikali vinafanya kazi kwa ushirikiano na kwamba pale inapohitajika mambo.ya kujadiliana wasisite kufanya hivyo ili kuongeza ari ya utendaji ili kuinua uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya uwezeshaji Asasi za kiraia (FCS), Francis Kiwanga amesema AZAKI ipo kwa ajili ya ujenzi wa mambo chanya ya kimaendeleo na kuhidumia jamii na kwamba wataendelea kutoa ushirikiano kwa serikali katika mambo mablimbali.

Wiki ya asasi za kiraia (AZAKI) ilifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa Novemba 4, 2019 Jijini Dodoma na kuhitimishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo hii leo Novemba 8, 2019.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Novemba 9, 2019
Alichokizungumza Prof. Kabudi na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Finland na Denmark

Comments

comments