Meneja wa klabu ya Man Utd  Jose Mourinho huenda akakumbana na adhabu ya kufungiwa michezo minne, kufuatia utovu wa nidhamu aliouonyesha wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Burnley.

Gazeti la The Sun limeandika taarifa zinazodai kuwa, kamati ya nidhamu ya chama cha soka nchini England (FA), imekutana na kupitia ripoti ya mwamuzi Mark Clattenburg na kubaini kulikua na ukiukwaji wa kanuni ambao ulifanywa na meneja huyo kutoka nchini Ureno.

Uvunjwaji wa kanuni za benchi la ufundi ambazo zilifanywa na Mourinho hadi kusababisha kutolewa eneo la utendaji wa kazi zake na kuamuriwa kukaa jukwaani, umeifikia kamati hiyo huku akiwa na kesi nyingine ya kushinikiza mwamuzi  Anthony Taylor kubadilishwa wakati wa mchezo dhidi ya Liverpool ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Kwa makosa hayo mawili Jose Mourinho yupo katika hali ngumu ya kujitetea kutokana na ushahidi ambao umeshawasilishwa mbele ya kamati ya nidhamu, lakini kabla ya kutolewa maamuzi ya kufungiwa atapewa nafasi ya kujitetea.

Faraja Kotta aumizwa na kinachomkuta Miss Tanzania Mpya, akumbuka machungu
Frank de Boer Kusubiri Hatma Yake Inter MIlan