Joto la uchaguzi nchini Marekani limezidi kupanda huku Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump akiendelea kupata uungwaji mkono, huku Hillary Clinton wa Democratc naye amekuwa akifanya mikutano mabali mbali katika majimbo ambayo ni  ngome ya chama cha Democratic.

 Ikiwa zimebakia siku tatu pekee kabla ya upigaji kura mawakili wa chama cha Democratic wamefungua kesi mahakamani dhidi ya mawakala  wa Donald Trump kwa kuanzisha mtindo wa kuhakiki wapiga kura siku ya upigaji kura.

Trump ametoa wito kwa mawakili wake kutekeleza majukumu yao vizuri wakati wa uchaguzi ili waweze kuhakikisha kura haziibiwi na upande wa chama cha Democratic.

Katika jimbo la Ohio, Jaji ametoa amri dhidi ya kundi la kampeni la Donald Trump lihakikishe kuwa halishiriki katika kuwatisha watu wanaotaka kupiga kura.

Wakati huohuo Bi Clinton ameungana na mwanamziki  wa Rap, Jay Zee katika hafla maalum iliyokuwa  kwaajili ya kuomba uungwaji mkono kwa wapiga kura wenye asili ya Afrika wajitokeze kwa wingi Jumanne kupiga kura

Vuguvugu la Trump, Clinton kuingia 'White House' lapamba moto
Lissu aanzisha mgomo nje ya mahakama, adai hana barua