Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa hatajali maneno ya watu ambao watasema kuwa yeye anajenga miundombinu kwenye Mkoa anaotoka Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa, kwa kuwa anajua alipotoka naye.

Ameyasema hayo mkoani Mtwara wakati akizindua Kituo cha Afya Mbonde kilichopo Masasi, ambapo amesema kuwa wapo watu watasema kuwa anajenga sehemu anayotoka rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa sababu bila yeye asingekuwa waziri au Rais.

”Wapo watakaosema ninamjengea Mkapa, ndiyo namjengea Mkapa, kwa sababu bila Mkapa mimi nisingekuwa Waziri inawezekana pia Urais msingeniona, sasa kumjengea barabara tu hata siku akienda kuzikwa apite kwenye lami ni kosa?, najua Mkapa amenitoa wapi,”amesema Rais Magufuli

Kuhusiana na Waziri wa awamu ya tatu kupewa kiwanda cha korosho lakini hakiendelezi, Rais Magufuli ameagiza kunyang’anywa kwa kiwanda hicho na kama akikataa akamatwe na apelekwe mahakamani hata kama alikuwa waziri kwani awamu hii haibembelezi mtu.

Hata hivyo, Rais Magufuli ametoa wito kwa waliouziwa viwanda vya kubangua Korosho na Serikali, kwamba ni lazima waanze kubangua Korosho na wazinunue, wakishindwa wavirudishe viwanda, huku akimuagiza waziri wa kilimo kumnyang’anya mmiliki wa kiwanda kilichopo Newala.

  • Hukumu ya Lema yatajwa
  • Upinzani wasusia bunge hukumu ya Lema, watoka nje
  • Maonyesho ya TAFITI UDSM yaanza rasimi

 

 

 

Mwanamke alijifungua juu ya mti akikwepa Kimbunga Idai
RC Mtaka azindua kambi za kitaaluma mkoani Simiyu

Comments

comments