Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewataka wakulima nchini kupandisha bei ya mazao kadri watakavyo kutokana na nguvu kubwa wanayoitumia katika uzalishaji  wa mazao hayo.

Amesema hayo mara baada ya kuwepo malalamiko ya kupanda kwa bei za mazao mbalimbali  hasa mahindi na mchele kutokana na upatikanaji wake kuwa mdogo.

“Wakulima pandisheni bei ya mazao kwa kiwango mnachotaka bila kuzuiliwa na mtu wala kiongozi yeyote wa serikali, mmekuwa mkipata shida nyingi kuhangaika hadi kuzalisha mazao hayo, huu ni mwaka wa neema kwa wakulima, tumieni fursa hii pandisheni bei za mazao kadri mnavyotaka,”amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewataka watu wanaolalamika kupanda kwa bei za vyakula na mazao mbalimbali wakalime wenyewe shambani ili wakapate machungu wanayopata wakulima.

Hata hivyo Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Shinyanga kwa kutekeleza kauli mbiu ya Hapa Kazi tu, kwa kuhakikisha wanalima kwa kiwango kikubwa na kuwasihi watumie mvua zilizopo kuzalisha mazao kwa wingi.

Dimitri Payet Ashinikiza Kuondoka West Ham Utd
Morgan Schneiderlin Atua Rasmi Goodison Park