Klabu ya Everton imekamilisha usajili wa kiungo kutoka nchini Ufaransa Morgan Schneiderlin, akitokea Old Trafford yalipo makao makuu ya ya Man Utd.

Everton wamekamilisha usajili huo, kwa ada ya Pauni milioni 20 na wamemsainisha mkataba wa miaka minne na nusu.

Haikuwa rahisi kwa The Toffees kukamilisha mpango wa kumuhamishia Schneiderlin huko Goodson Park, kwani iliwalazimu kuomba kupunguziwa ada ya uhamisho ambayo ilikua Pauni milioni 24.

Uhamisho wa Schneiderlin kwenda Everton, umechangiwa na meneja Ronald Koeman, ambaye aliwahi kufanya kazi na mchezaji huyo wakiwa kwenye klabu ya Southampton.

Schneiderlin aliondoka St Mary’s na kuelekea Old Trafford mwaka in 2015, lakini alishindwa kumshawishi meneja wa sasa wa Man Utd Jose Mourinho, tangu alipowasili klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu.

Kwa msimu huu alibahatika kucheza michezo minane pekee akiwa na Man Utd, na tangu mwezi Novemba hakuwahi kujumuishwa kwenye kikosi cha mashetani hao wekundu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, alijiunga na Man utd wakati wa utawala wa meneja aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita Louis Van Gaal.

Schneiderlin anakua mchezaji wa pili kusajiliwa na klabu ya Everton katika kipindi hiki cha dirisha dogo, akitanguliwa na kinda lenye umri wa miaka 19 Ademola Lookman likitokea Charlton.

JPM: Wakulima pandisheni bei mtakavyo
Mwana FA ataja kosa kubwa linalofanywa na wasanii wa Bongo Fleva