Wakala wa mshambuliji kutoka nchini Hispania na klabu ya Real Madrid  Alvaro Morata, ameonyesha matumaini ya kufanyika kwa biashara ya uhamisho wa mchezaji wake ambaye, anahitajika kwenye himaya ya Jose Mourinho.

Juanma Lopez wakala wa mshambuliaji huyo, amesema kuna uwezekano wa mazungumzo kati ya Man utd na uongozi wa Real Madrid kuhusu uhamisho wa mchezaji wake kuanza wakati wowote kuanzia sasa.

Man Utd tayari wameshatuma ofa ya Pauni million 52, kwa ajili ya uhamisho wa Morata, lakini uongozi wa Real Madrid umekua kimya pasina kusema lolote kuhusu ofa hiyo.

Hata hivyo Los Blancos wameripotiwa kuikataa ofa hiyo, na mapendekezo yaliyotolewa na viongozi wa bodi yatailazimu Man Utd kuongeza dau na kufikia Pauni milioni 78, ili kufanikisha mpango wa kuondoka kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

Wakati huo huo wakala wa Morata amesema, mbali na Man utd kuonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji wake, pia klabu ya AC Milan ya Italia imeonyesha kufanya hivyo, jambo ambalo huenda likaongeza thamani ya usajili.

Morata alirejea Real Madrid akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC mwishoni mwa msimu wa 2015/16, na ameifungia Los Blancos  mabao 20 katika michezo yote aliyocheza msimu wa 2016/17.

Watano Kusajiliwa Stamford Bridge
Irene Uwoya afunguka kuhusu ombi la Dogo Janja kummiliki