Jukwaa huru la wazalendo limelaani kitendo cha meya wa jiji la Dar es salaam ndg Mwita Waitara cha kuwapotosha kwa makusudi wanainchi wa Dar es salaam na taifa kwa ujumla kuhusu agizo la  mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Makonda la kuchukua taarifa za kila kaya.
Hayo yamesemwa na Mw/kiti wa jukwaa hilo Bw,Andrew Kadege alipokuwea akiongea  na waaandishi wa habari jijini Dar es salaam mapema hii leo,na kuongeza kuwa jukwaa limesikitishwa sana na kuibuka kwa ndugu Mwita na harakati za kupinga hatua hiyo nzuri ya Mh, Makonda kutaka kujua taarifa za kila kaya.
Aidha alionngeza kuwa harakati za kisiasa za ndg Mwita zimemshtusha ata mlezi wa chama hicho ndg Edward Lowasa na kukemea siasa za kiharaakati ambazo zinapinga maendeleo ya nchi,’’jukwaa linakemea vitendo aambavyo vinarudisha nyuma jitihada za serikali ya awamu ya tano na kuchelewesha uhakiki wa wanai nchi wake’’ alisema Bw, Kadege.
Hata hivyo jukwaa imemtaka meya kutokuendelea na tabia ya kuwalaghai wanainchi kutoshiriki katika shughuli za maendeleo kwani ndio sehemu yao ya kujikwamua kiuchumi na kuondoa umasikini unaowakabili watanzania kwa ujumla.
Jukwaa limeongeza kuwa hatua hiyo ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ya kutaka kuwatambua wainchi wa mkoa wake wa Dar es salaam katika ngazi ya kaya ni kutaka kujua jinsi gani ya kuweza kupanga na kuwahudumia kama ilivyo katika majiji ya London,Paris na Berlin inavyofanyika.
Jukwaa huru limechukua nafasi hiyo kuwaomba na kuwashauri wanainchi wote popote litakapo fanyika zoevzi hilo kushirikiana na serikali kikamilifu kwani ni kwa manufaa ya wainchi wenyewe na taifa kwa ujumla ili kuweza kuinua uchumi.