Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imesema kuwa imefarijika pakubwa kuona rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akinunua ndege mpya na kutimiza ilani ya chama hicho.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Dkt. Edmund Mndonwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa hatua ya kununua ndege hizo mpya zitaiwezesha nchi kuingia katika soko la ushindani wa kibiashara.

”Kwa hatua hii ya rais Dkt. Magufuli ambaye ni mwenyekiti wetu taifa, inaliweka taifa katika ramani ya ushindani wa kibiashara, kitu ambacho tulikuwa tumeshapotezwa kabisa na mataifa mengine ya jirani, na hii itarahisisha hata usafiri wa ndani ya nchi kwa maeneo ambayo yalikuwa hayafifi kirahisi nasasa yatafikika,”amesema Dkt. Mndonwa

Atashasta akanusha tuhuma za kuihujumu FASTJET 'Wanamatatizo yao'
Video: Mbivu, mbichi muswada wa vyama vya siasa Jumatatu, Polisi wa dhahabu wafukuzwa kazi

Comments

comments