Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati 2021 (KAGAME CUP), inaanza rasmi leo Jumapili (Agosti Mosi) jijini Dar es salaam.

Michuano hiyo itaanza kuunguruma katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mchezo wa Kundi A kuchezwa ambapo wenyeji Young Africans watajitupa kwenye dimba hilo mishale ya saa moja jioni kupambana na waalikwa Nyasa Big Bulltes kutoka Malawi.

Hata hivyo waandaaji wa michuano hiyo wamethibitisha kufanya mabadiliko ya ratiba kwa kuahirisha mchezo wa Express ya Uganda dhidi ya Altabara ya Sudan Kusini uliokuwa uanze mapema kabla ya mchezo wa pili wa kundi A.

Taarifa kutoka CECAFA imeeleza kuwa kwa mwaka huu michuano hiyo itaanza kwa kupigwa kwa mchezo mmoja kati ya wenyeji Young Africans dhidi ya waalikwa Big Bullets FC kutoka Malawi jumapili ya leo.

Mchezo huo umesogezwa mbele kutoka saa 10:00 jioni na sasa itapigwa saa 1:00 usiku.

Mchezo kati ya timu ya Express ya Uganda dhidi ya Atlabara kutoka Sudan Kusini uliotakiwa kuchezwa leo Jumapili umesogezwa mpaka kesho Jumatatu.

Young Africans yamshusha pacha wa Miquissone
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 1, 2021