Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) inaanza rasmi Agosti Mosi ikifanyika nchini Tanzania na tayari ratiba rasmi imeshatoka leo huku klabu za Tanzania zikipangwa na vigogo wengine.

Ratiba hiyo inaonyesha Agosti Mosi, KCCA watafungua dimba kwa kucheza na KMKC katika uwanja wa Chamazi, Agosti 2 Azam FC wataikaribisha Tusker FC katika uwanja huo huo.

Wakati Azam ikicheza upande wa Yanga wao watashuka dimbani kwenye uwanja wa Mkapa wakicheza na Express Fc na Agosti 3 timu ya Le Messager itacheza na KCCA katika uwanja wa Chamazi.

Agosti 4 Altabara itacheza na Azam FC katika uwanja wa Chamazi wakati huo huo Nyasa Big Bullets itaikaribisha Yanga mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kisha mechi zitamaliziwa Agosti 5 na 6, KMKM wakicheza na Le Messager uwanja wa Chamazi na Agosti sita Tusker na Altabara kwenye uwanja wa Chamazi huku Express wakicheza na Nyasa Big Bullets uwanja wa Taifa.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 29, 2021
Ripoti uchunguzi vifo vya samaki ufukweni