Rapa nyota wa mziki wa kufokafoka, Khaligraph Jones amefichua mipango ya kurejea darasani kuendela na masomo yake baada ya kumaliza Kidato cha nne miaka mingi iliyopita.

Msanii huyo ambaye hutambulika kwa msemo wa ‘Respect The OG’ alifichua kuwa anapania kurejea shuleni ili kusomea sheria na katiba kwa kuwa ana mipango ya kujishughulisha na mambo tofauti mwaka 2027 baada ya kumaliza kozi hiyo.

Katika mahojiano ya awali, Khaligraph alifichua kuwa maisha yake ya utotoni yalikuwa magumu na hivyo kumzuia kujiunga na chuo kikuu baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari.

Wakati huo huo rapa Jones, kupitia ukurasa wake wa Instagram, amefichua kuwa ataachia kibao chake kipya cha injili ‘Sifu Bwana’ siku ya Ijumaa, Januari 21, 2022, baada ya video fupi inayomuonyesha akirap wimbo huo kusambaa na kupokelewa vyema na mashabiki wake.

Hofu yatanda, Miili yaendelea kuopolewa mtoni
Mchakato wa Urais Kenya; wasaliti wa Chama tawala wapata Kiboko cha Rais