Kampuni ya Coca-Cola imetangaza mpango wa kutengeneza kinywaji chenye kilevi kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 125 ya Kampuni hiyo nchini Japan.

Bidhaa hiyo ya muundo wa alcopop inatarajiwa kuwa na kiwango cha kileo chenye ujazo wa kuanzia asilimia 3% hadi 8%.

Aidha, Rais wa Coca-Cola nchini Japan, Jorge Garduno amesema kuwa hawajawahi kujaribu kutengeneza bidhaa kama hiyo yenye kileo kidogo, lakini wanaangalia namna ya kutumia fursa.

Hata hivyo, Kampuni kubwa za vinywaji nchini Japan ikiwemo Kirin, Suntory na Asahi zina aina mbalimbali za vinywaji na wameendelea kufanya majaribio mbalimbali.

Rais Buhari awataka viongozi wa Afrika kuiga mfano kwa Ghana
Simba yatoa utaratibu kwa wanaotaka kwenda Misri