Beki wa Kulia wa Simba SC Shomari Salum Kapombe amesema bado wanaendelea kupambana katika michezo ya Ligi Kuu, ili kufikia lengo la kutetea Ubingwa wao, licha ya kuachwa kwa tofauti ya alama 08 na Young Africans.

Kapombe ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Simba SC kilichocheza dhidi ya Kagera Sugar jana Jumatano (Mei 11), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam amesema, siku zote mtafutaji hana sifa ya kuchoka, hivyo kama wachezaji wataendelea kufanya majukumu yao.

Amesema Ligi ni mchezo wa kupambana bila kukata tamaa, hivyo Mashabiki na Wanachama wa Simba SC wanapaswa kuendelea kuwaamini wachezaji wakati wote.

“Tumeshinda dhidi ya Kagera Sugar, ulikua mchezo wa kulipa kisasi kwa sababu walitufunga kwao na tukaangusha alama ambazo zinatusumbua kwa sasa kwa sababu tumeachwa na wanaoongoza Ligi kwa alama zao, lakini bado tunapambana hatujakata tamaa.”

“Wachezaji wa Simba SC tumekubaliana kupambana hadi mwisho wa msimu huu, ili kuangalia nini tutakachokipata, Mashabiki na Wanachama wanapaswa kuendelea kutuamini ili tukamilishe kazi ili mbele yetu.” amesema Kapombe

Ushindi wa 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, unaendelea kuiweka Simba SC nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 49, huku ikitanguliwa na Young Africans yenye alama 57 kileleni.

Ahmed Ally: Nisiwe mnafiki tunawaombea mabaya
Kaduguda amaliza utata sakata la Morrison