Nahodha na mlinda mlango wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni ( KMC FC) Juma Kaseja pamoja na David Brayson wameungana  na wachezaji wenzao leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu Soka Tanzania bara ikiwa ni baada ya kutoka katika kikosi cha Timu ya Taifa Taifa Stars katika mchezo wa kufuzu kombe la Afrika (AFCON 2021).

Mbali na Kaseja na Brayson, wengine waliorejea kuungana na kikosi cha KMC FC ni Kocha wa Makipa wa timu hiyo, Fatuma Omary ambaye aliitwa kufundisha makipa wa Timu ya Taifa ya Wanawake U-17 katika michuano ya kuwania ubingwa wa kombe la COSAFA.

Kikosi cha KMC FC kinajiandaa na mchezo wa mzunguko wa 12 wa Ligi Kuu Tanzinia Bara, ambapo itakutana na Azam FC Jumamosi Novemba 21, kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wenyeji wa mchezo huo.

Hata hivyo katika kikosi hicho, wachezaji wawili bado hawajarejea kambini ambao ni Kenny Ally ambaye alifiwa na Baba yake mzazi pamoja na Rahim Sheihe ambaye bado yupo katika Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes.

Hadi sasa kikosi cha KMC FC hakina majeruhi na kwamba mchezaji ambaye alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Gwambina Misungwi Mkoani Mwanza , Emmanuel Mvuyekule amesharejea mazoezini na kwamba anaendelea vizuri hadi.

Nabii Bushiri ajisalimisha kwa polisi
DRC yatangaza kumalizika kwa Ebola