Chama cha mawakili nchini Kenya LSK kimemkosoa rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta dhidi ya matamshi yake ya kuwashambulia majaji wa mahakama Kuu kufuatia uamuzi wa kubatilisha matokeo ya uchaguzi yaliyompatia ushindi.

Rais wa Chama cha Mawakili nchini humo LSK,  Isaac Okero amemkosoa Rais huyo mara baada ya kumtaja jaji mkuu wa mahakama kuu nchini humo, David Maraga na majaji wengine wa mahakama hiyo kuwa ni wakora

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wafuasi wake jijini Nairobi mara baada ya mahakama nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu nchini humo ambapo amewatupia lawama majaji kwa kuchukua uamuzi huo.

”Haki yake inafaa kuheshimu, kukubali na kulinda haki za jaji mkuu na kila jaji wa mahakama kuu  chini ya kifungu cha sheria cha 28,”amesema Okero.

Hata hivyo, Kiongozi huyo wa LSK amesema kuwa mahakama hiyo imetekeleza wajibu wake na kuwaonya viongozi wengine dhidi ya kuwatishia majaji

Mwanahabari Muhingo Rweyemamu afariki dunia
Video: Jaji David Maranga ''Mimi si mradi wa Serikali''