Vinara wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza Man City, wataingia katika kipindi cha majaribu ya kucheza bila ya kiungo mshambuliaji wao kutoka nchini Ubelgiji Kevin de Bruyne, kuanzia mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Celtic utakaounguruma siku ya jumatano.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, alilazimika kutoka uwanjani katika dakika ya 81 wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Swansea City uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita katika uwanja wa Liberty na vinara hao kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.

Taarifa za awali za kitabibu zinaeleza kuwa, De Bruyne huenda akawa nje ya uwanja kwa muda wa majuma mnne, lakini meneja wa Man City Pep Guardiola amesisitiza kusubiri majibu ya vipimo.

“Hatuwezi kujua kwa undani nini tatizo linalomsumbua, unaweza kukuta ni maumivu ya misuli. Hivyo ningependa kuwaambia wahusika wa Man city kusubiri majibu ya vipimo,”

“Natambua De Bruyne ana umuhimu mkubwa katika kikosi cha Man City, lakini kama itatokea majibu yanakuja tofauti sina budi kutafua mbinu mbadala kwa sababu nina kikosi kipana.” Alisema Guardiola.

Majaliwa azindua mfumo wa tiketi za kielektroniki kuingia uwanja wa Taifa
Slaven Bilic: Haya Ni Mapito, Tutarudi Njia Kuu