Mwanamuziki staa wa Bongoflava, Alikiba maarufu kama ‘King Kiba’  ameshitakiwa na mwanamke mmoja kutoka Mombasa kwa madai ya kuwa amepewa mimba na msanii huyo na  mara baada ya kuzaa amemkimbia, hivyo ujio wake ni kumtaka kumpa mtoto wake matunzo.

Inasemekana mwanamke huyo amefunga safari toka Mombasa Kenya hadi Tanzania kumtafuta baby dady wake baada ya Alikiba kushindwa kupatikana kwa njia ya Simu.

Mwanamama huyo amezungumza amesema mimba hiyo imepatikana kipindi ambacho msanii pendwa Alikiba alipoenda Mombasa kufanya show.

Alikiba ametafutwa kutoa maelezo juu ya madai ya huyo mwanamke wa Mombasa naye amejibu kwa kusema ili kudhibitisha kuwa mtoto wake ni lazima akapime damu (DNA).

Mazungumzo hayo yamefanyika katika kipindi cha XXL leo.

Kaimu Jaji Mkuu awapa neno mawakili, ataka haki itendeke katika jamii
Video: 'Tumechoka matapeli, sasa Serikali tumeamua tufike' - Rais Magufuli