Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Khamis amewataka mawakili kutumia taaluma yao waliyonayo kutoa msaada wa kisheria katika jamii.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kuwaapisha na kuwapokea mawakili wapya 248, ambapo amesema kuwa mawakili wapya wanatakiwa kutenda haki katika shughuli zao.

“Mawakili wote wanatakiwa kuwa waaminifu kwa wateja wanaowahudumia na kushirikiana na mahakama katika kutoa haki na wasiwe mawakala wa rushwa bali wawe mawakala wa kutenda haki,”amesema Prof. Khamis.

Aidha, Kaimu Jaji Mkuu amewataka mawakili hao kufika nje ya mji ili kuweza kutoa msaada wa kisheria katika jamii kwa kuwa kumekuwa na changamoto kubwa katika maeneo hayo.

Hata hivyo, kwa upande wake Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS), Tundu Lissu amewataka wanasheria hao kutumia taaluma zao kuisadia jamii katika kupata haki.

Mbowe afafanua malalamiko yake kuhusu Lowassa kuitwa Polisi
Kiba adai kusingiziwa mtoto na mwanamke wa kimombasa, ahoji majibu ya DNA