Mshambuliaji mpya wa klabu iliyorejea ligi kuu msimu huu Coastal Union, Ali Saleh Kiba amejiunga na kambi ya timu hiyo iyopo mkoani Tanga.

Kiba anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi hicho kitakachocheza mchezo wa tatu wa ligi kuu Tanzania bara (TPL) dhidi ya KMC Jumamosi ya Septemba 1 saa nane mchana katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kiba ambaye anafahamika zaidi kama Mwanamuziki kutokana nakufanya vizuri katika fani hiyo, ikiwa ni pamoja na kutwaa tuzo ya Msanii bora wa Afrika kupitia tuzo za muziki za MTV Europe mwaka 2016, amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu hiyo sambamba na kuwa mmoja ya wadhamini kupitia kinyaji chake cha MoFaya.

Aidha, Ali Kiba alikosa mechi mbili za mwanzo kufuatia kuwepo nchini Canada kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki. Katika michezo hiyo ya mwanzo Coastal union imefanikiwa kukusanya pointi 4 baada ya kutoka sare mchezo mmoja dhidi ya Lipuli na kushinda dhidi ya Biashara United.

Shujaa wa Marekani atundika daruga rasmi
Sakata la Mtawa kujiua laibua sura mpya, Kamanda atoa ufafanuzi