Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameungana na Marais wengine Wastaafu wa Afrika kushiriki katika Mkutano wa Jukwaa la 7 la Uongozi Afrika (ALF 2023). Mkutano huo umefanyika katika Jiji la Accra, Ghana miaka minne baada ya kufanyika mara ya mwisho mwaka 2019. 

Mkutano huo wenye mada “kukuza biashara ya baina ya nchi za Kiafrika ili kufungua fursa zitokanazo na kilimo” umeratibiwa kwa pamoja kati ya Taasisi ya Uongozi ya Tanzania (Uongozi Institute) na Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AFCFTA). Rais Kikwete ni Mlezi wa Jukwaa hilo la Uongozi Afrika, alichukua nafasi hiyo kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Tatu wa Tanzania, Hayati Benjamin Mkapa.

Mkutano huo unaelezwa kufanyika kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuhudhuriwa na idadi kubwa zaidi ya Viongozi Wastaafu wa Afrika wakiwemo Olisegun Obasanjo wa Nigeria, Mohamed Moncef Marzouki wa Tunisia, Goodluck Jonathan wa Nigeria na Thomas Bon Yayi wa Benin.

Wengine ni Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone, Hailemariam Desalegn wa Ethiopia na Ellen Sirlief Johnson wa Liberia. Aidha, Katibu Mkuu wa AFCFTA, ambayo ndiyo Taasisi ya Kibara iliyopeeq jukumu la kukuza biashara baina ya nchi za Kiafrika na kuongeza kiwango cha biashara ya Afrika katika masoko ya Dunia pia amehudhuria.

Jukwaa la ALF, linasifika kuwa Jukwaa pekee katika Bara la Afrika ambalo linatoa fursa kwa Viongozi Wastaafu wa Nchi na Serikali kujumuika kwa pamoja na kujadiliana kwa uwazi juu ya changamoto mbalimbali zinazolikabidi bara la Afrika. Viongozi hupata fursa ya kutoa mapendekezo na ushauri kwa Viongozi wa sasa waliopo madarakani kwa lengo la kuboresha maslahi ya nchi na watu watu wa Afrika.

Miongoni mwa masuala yaliyojitoleza katika majadiliano hayo ni kwa Serikali kuweka mikakati na kufanya jitihada za dhati kutambua nafasi ya vijana wa kiafrika katika kukuza sekta ya kilimo ambayi ndiyo inayotoa ajira nyingi kuliko sekta zote.

Aidha vikwazo vinavyokwamisha ushiriki wa vijana katika kilimo vilijadiliwa kwa kina, huku Mpango wa Serikali ya Awamu ya Sita wa BBT (Build Better Tomorrow) ukisifiwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa na nchi nyingine za kiafrika. Mpango wa BBT unalenga kumsaidia kijana kupata ardhi, pembejeo na mtaji wa kufanya kilimo.

Vifo vya mfungo Kenya: Majambazi wenye silaha walisimamia zoezi
Dickson Job apewa tuzo mchezaji bora Ligi Kuu