Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania bara (Kilimanjaro Queens) imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Afrika mashariki na kati kwa kuifunga timu ya taifa ya Kenya katika mchezo wa fainali uliomalizika muda mchache uliopita mjini Jinja nchini Uganda.

Kilimanjaro Queens wametimiza azma ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza chini ya usimamizi wa baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA, kupitia mabao yaliyofungwa na Mwanahamis Omar.

Hata hivyo kabla ya michuano hiyo kuanza, timu ya taifa ya Tanznaia bara ilikua inatajwa huenda ingefanya vyema kufuatia kuwa na wachezaji wenye uzoefu, tofauti na timu za mataifa mengine yaliyoshiriki.

Kitendo cha Kilimanjaro Queens cha kutwaa ubingwa wa michuano hiyo, huenda kikawa faraja kwa ndugu zao wa Zanzibar (Zanzibar Queens) ambao wameandika historia ya kufungwa mabao 30 katika michezo mitatu waliyocheza kwenye hatua ya makundi.

Zainzibar Queens ilikua inanolewa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Twiga Stars) Nasra Juma, jambo ambalo lilitoa mwanya kwa Kilimanjaro Queens kuongozwa na kocha Sebastian Nkoma.

Wakati huo huo timu ya taifa ya Ethiopia imefanikiwa kuchukua nafasi ya tatu, baada ya kuifunga timu ya taifa ya Uganda mabao manne kwa moja.

Marekani Yalaani Shambulio lililotokea nchini Syria
Pep Guardiola: Yaya Toure Hatocheza Tena Man City