Wakazi zaidi ya 200 wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara wamenufaika na huduma ya matibabu ya kliniki tembezi iliyotolewa  kwa siku tatu na wataalamu wa kibigwa wa Hospitali ya Bejamini Mkapa (BMH).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano, huduma ya kliniki tembezi ilijumuisha utoaji wa huduma za kibigwa kwa magonjwa ya moyo, figo na mfumo wa mkojo na upasuaji.

Naye Mganga mkuu wa wilaya ya kiteto Dkt. Pacshal Mboto ametoa shukrani kwa madktari bigwa kutoka katika hospitali ya Mkapa kwa kusaidia watu ambao walikuwa wakikosa huduma za kibigwa kama hizo.

Dkt. Mboto amesema kuwa mpango huo pia umesaidia Hospitali ya wilaya kuongeza mapato ya ndani kwa siku tatu za huduma na kusisitiza haja ya ushirikiano wa kudumu katika utoa huduma kati ya BHM na hospitali ya Kiteto

Amesema kuwa muda wa siku tatu wa kutoa huduma za kibigwa za kliniki tembezi haukutosha kutokana na idadi kubwa ya watu.

Naye Sufiana Rajabu (83) mkazi wa eneo la kibaya kata ya kibaya amabye amefanyiwa upasuaji wa njia ya mkojo wakati wa utoaji wa huduma ya kliniki  tembezi amesema kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa takribani miezi 6.

Alichokisema Lugola baada ya kung'olewa
Mchungaji amchoma moto mwanaye mwenye utindio wa ubongo