Baada ya kuanza vibaya michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kufunga mabao 3-1 ugenini dhidi ya Azam FC, Kocha Mkuu wa Horseed FC, Mohamed Hussein Ahmed amesema kuwa hawakuwa na cha kufanya kwa kuwa walizidiwa na wapinzani wao.

Horseed FC ilipoteza mchezo huo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali siku ya Jumamosi (Septemba 11), katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Kocha Mohamed amesema wenyeji wao walikua na kiwango kizuri, hasa baada ya kuwatangulia kufunga bao, lakini dakika chache baadae mambo yaliwabadilikia na kujikuta wakizidiwa, hali ambayo ilitoa mwanya kwa Azam FC kupata ushindi wa mabao 3-1.

“Bahati mbaya sana kwetu tulizidiwa na wapinzani wetu kipindi cha pili lakini kipindi cha kwanza mambo yalikuwa sawa tulijitahidi. Azam FC ni timu nzuri hivyo kwa walichotuonyesha ni funzo kwetu ili tujipange zaidi kwa mchezo wetu ujao,” amesema.

Wakati huo huo Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amesema kuwa uwezo wa wachezaji pamoja na kambi ambayo waliifanya nchini Zambia ni moja ya sababu ya wao kuweza kushinda.

“Ukitazama mchezo ulikuwa mgumu na kila timu ilikuwa inahitaji ushindi, kwa kilichotokea ni pongezi kwa wachezaji kwani walifanya kile ambacho tuliwaambia. Kambi ya Zambia na maandalizi mazuri yametupa matokeo ila bado kazi inaendelea,” alisema.

Mchezo wa mkondo wa pili kati ya klabu hizo unatarajiwa kuchezwa Septemba 18, Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam ila wenyeji watakuwa ni Horseed FC kutoka Somalia.

Waziri Aweso aitumia Bashungwa Cup kuwapa mbinu wabunge
Mwakalebela afichua siri ya kichapo Young Africans