Kocha cha msaidizi wa Young Africans Juma Mwambusi, amewasilisha maombi kwa uongozi wa klabu hiyo, akitaka kujiweka pembeni kwa muda.

Hatua hiyo imefikia baada ya yeye mwenyewe kuandika barua baada ya kikosi hicho kutwaa taji la Mapinduzi ambapo iliifunga Simba kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana, Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar.

Mwambusi ambaye alirejea klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu, akifanya kazi na kocha mkuu Cedric Kaze, amewasilisha maombi hayo kwa mabosi wake, kufuatia matatizo ya kiafya yanayomkabili.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans, Mshindo Msolla amesema kuwa, kwenye barua yake ya kuomba kujiweka kando ametaja sababu kuwa ni kuwa na matatizo ya kiafya.

Kocha Juma Mwambusi.

Ameongeza kuwa ameshauriwa na wataalamu kukaa sehemu ambayo itamfanya asiwe na msongo wa mawazo pamoja na kupiga kelele.

Kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze raia wa Burundi ambaye ameachiwa jukumu la kusaka msaidizi wake.

Juma Mwambusi aliwahi kufanya kazi Young Africans wakati wa kocha Mholanzi Hans Van Der Pluijm, na baadae aliondoka na kocha huyo alipoajiriwa Azam FC.

Pitso Mosimane amtema Geraldo da Costa
TPLB: Ligi Kuu Kuendelea Februari 13