Mwanamuziki maarufu nchini Marekani, Kodak Black ameingia tena kwenye mkono ya sheria akiwa anaelekea kutumbuiza kwenye tamasha la Rolling Lound usiku wa kuamkia leo kwa makosa ya silaha.

Imeripotiwa kuwa baada ya uchunguzi wa muda mrefu rapa huyo alikamatwa na vikosi vitatu, shirika la pombe, Tumbaku na silaha ATF pia walikuwepo Miami -Dade Police Northside Gang Unit, pamoja na U.S Marshals tayari amefikishwa kwenye jela ya kijajusi mjini Miami.

Matatizo ya kisheria yamezidi kumuandaa rapa Kodak Black baada ya kukamatwa siku kadhaa zilizopita akiwa na silaha pamoja na dawa za kulevya kwenye gari lake.

Hata hivyo kodak amekuwa akikamatwa mara kadhaa na askari na kukutwa na silaha kinyume cha sheria huku akisitisha mara kadhaa ziara zake za muziki.

 

 

Askofu Kakobe amkingia kifua Askofu Gwajima
Mabasi ya mwendokasi yasitisha safari zake, barabara zafungwa

Comments

comments