Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemfikisha mahakamani mfanyabiashara Benedict Kimbusu mkazi wa Kinondoni kujibu shitaka la kusambaza maudhui mtandaoni bila kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Kimbusu alifikishwa mahakamani hapo leo na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi MkaziMwandamizi Yusto Luboroga.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali, Aldoph Ulaya alidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya Februari 27, 2014 hadi Desemba 7, 2020 katika maeneo tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam Kimbusukupitia mtandao wa kijamii wa Youtube alichapisha maudhui bila leseni ya TCRA.

Ilidaiwa mshitakiwa huyo alitumia akaunti yenye jina la ‘Pioh the 90s Lyrics’ kwenye mtandao ya youtube kusambaza maudhui hayo.

Kimbusu alikana shtaka hilo.Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 30, 2020 kwa kuwa upande wa mashtaka ulidai upelelezihaujakamilika na waliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Mshitakiwa huyo aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya dhamana ya Sh milioni tatu kila mmoja.

Namungo FC yaweka kambi Zanzibar
Bocco atoa ahadi kabambe Simba SC