Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea amesema kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai hatoshi kuendelea na nafasi hiyo ya kuliongoza bunge kwani amekuwa akiwakandamiza wabunge wa Chadema.

Kubenea amemtuhumu Spika kuwa hafai kwa sababu pia alishawahi kupata kashfa ya kumpiga ndugu yake aliyekuwa mgombea mwenzake wa nafasi ya ubunge Jimbo la Kongwa Mkoani Dodoma.

Kwa mijibu wa taarifa hiyo kutoka katika gazeti la Nipashe, Kubenea ameyasema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara na wapiga kura wake wa kata ya Manzese Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa Ndugai alifanya tukio hilo wakati wa kinyang’anyiro cha kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Simshangai Ndugai kwa sababu alimchapa ndugu yake, Mgogo mwenzake, leo amewafungia wabunge wa upinzani akiwemo mbunge jimbo la Kawe, Halima Mdee na Ester Bulaya kutoshiriki vikao vya Bunge,”amesema Kubenea.

Hata hivyo, amewataka wapiga kura wake kutoshangaa kwa kukaa kimya kwa kila mradi katika Manispaa mpya ya Ubungo kwakuwa Manispaa hiyo bado mpya na kulikuwa mgawanyo wa miradi hiyo.

Prof. Mbarawa: wananchi waliopisha ujenzi wa barabara watalipwa kwa mujibu wa sheria
Kendrick Lamar amzawadia shabiki mlemavu toleo jipya la gari maalum

Comments

comments