Hali ya usalama kuelekea mchezo wa Jumamosi wa Clasico kati ya Real Madrid na Barcelona umepangwa kuimarishwa maradufu kufuatia tukio la mashabulio ya kigaidi lililotokea wiki iliyopita jijini Paris. 

Mchezo huo wa La Liga utaangukia ikiwa imepita wiki moja baada ya magaidi kushambulia maeneo kadhaa katika mji mkuu huo wa Ufaransa na kuuwa watu zaidi ya 129 na kuacha wengine mamia majeruhi.

Mchezo huo wa Classico utakaochezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu hauko katika mashaka ya kutochezwa lakini polisi jijini Madrid wataongezwa ili kuhakikisha usalama zaidi katika mchezo huo utakaozikutanisha klabu kubwa duniani. 

Polisi wamedai kuwa mpaka vyakula vitakaguliwa wakati wa kuingia uwanjani hivyo kuwataka mashabiki kutoa ushirikiano katika mchezo huo.

Rufaa Za Vigogo Wa FIFA, UEFA Zakwama
Licha Ya Vitisho Vya Ugaidi, Ligi Za Ufaransa, Hispania Kuendelea