Hofu imetanda miongoni mwa wachezaji na mashabiki wa Man City kufuatia kuumia kwa beki kutoka nchini Ubelgiji Vincent Kompany ambaye usiku wa kuamkia leo alionekana kwa mara ya kwanza akicheza msimu huu.

Kompany alilazimika kutoka uwanjani na kukiacha kikosi cha Pep Guardiola kikiwa na wachezaji kumi katika mchezo wa mzunguuko watatu wa michuano ya kombe la ligi ya EFL dhidi ya Swansea City.

Katika mchezo huo Man City walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Kompany, mwenye umri wa miaka 30, alionekana kuwa na majonzi wakati akitoka uwanjani, na hali hiyo ilitoa tafsiri kwa mashabiki wa Man City huenda wasimuone tena kwa kipindi kirefi kama ilivyokua msimu uliopita.

Hata hivyo meneja wa Man City Pep Guardiola alishindwa kueleza kwa undani taarifa za kuumia kwa beki huyo, alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo dhidi ya Swansea kumalizika huko Liberty Stadium kwa kusema hafahamu ni muda gani atashindwa kumtumia Kompany.

“Daktari amezungumza na Vincent naimani nitapata taarifa, lakini kwa sasa hivi ni vigumu kusema chochote,” alisema Guardiola. “Lakini naimani halitokua tatizo kubwa sana”.

Ljungberg: Wenger Amepata Dawa Ya Kumaliza Ukame
Video: Barcelona yaishindwa Atletico Madrid, Haya hapa magoli yote na highlights