Mabingwa wa soka nchini England, Leicester City wamekubali kumuuza mshambuliaji wao kutoka nchini Croatia, ambaye aliwagharimu kiasi kikubwa cha pesa katika usajili wake mwanzoni mwa msimu huu, Andrej Kramaric.

Leicester City wametoa baraka za kuondoka kwa Kramaric, baada ya kukamilisha mazungumzo ya biashara na uongozi wa klabu ya Hoffenheim ya nchini Ujerumani.

Kramaric alisajiliwa na The Foxes mwaka 2015, akitokea kwenye klabu ya  HNK Rijeka ya nchini Croatia kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 9.7, lakini mwezi januari alipelekwea kwa mkopo nchini Ujerumani katika klabu ya Hoffenheim.

Hata hivyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ameuzwa kwa bei ya hasara ya Pauni milioni 8, na amekubali kusaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Hoffenheim.

Kramaric, alilazimika kuondoka King Power Stadium wakati wa dirisha dogo la usajili, kufuatia kushindwa kupata nafasi ya kucheza kila mwishoni mwa juma, na hatua hiyo ilionekana kuwa kikwazo kwake kutokana na uwezo wa washambuliaji wengine klabuni hapo.

Uongozi wa Hoffenheim, umefikia maamuzi ya kumsajili moja kwa moja Kramaric, baada ya kuridhishwa na uwezo wake kisoka ambao ulisaidia kuinusuru klabu hiyo isishuke daraja msimu wa 2015-16.

Victor Wanyama Autikisa Uongozi Wa Southampton
Goal Line Technology Kutumika Copa America 2016