Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amemtaka Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mtungi kujitafakari, kwani amedai kuwa Jaji huyo amekuwa ni mpofu kwa mambo mabaya wanayofanyiwa watu wa upinzani nchini.

Ameyasema hayo baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwaandikia barua CHADEMA ambayo anadai inatuhuma mbalimbali pamoja na vitisho.

“Msajili wa Vyama vya Siasa amekosa sifa na uadilifu (moral authority) ya kunyooshea kidole CHADEMA au chama kingine chochote cha upinzani kuhusiana na jambo lolote linahusu Sheria ya Vyama vya Siasa na kanuni zake,”amesema Lissu

Aidha, amesema kuwa viongozi wa vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, wamekuwa wakiuawa, kutekwa nyara na kupotezwa, wamepigwa risasi katika majaribio ya kuuawa, wameteswa, wamekamatwa na kushtakiwa kwa kesi za uongo.

Pia, Lissu ameongeza kuwa Msajili Mutungi amekuwa bubu na kiziwi asiyesikia wala kukemea uonevu na ukandamizaji huo dhidi ya vyama anavyovisimamia.

Hata hivyo, Msajili Jaji Francis Mutungi aliiandikia barua CHADEMA kuhusu kufanya siasa za kibabe na vurugu na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa.

 

Meli nyingine 19 zapigwa faini ya mabilioni na Serikali
Magaidi washambulia kwa mabomu eneo la makazi ya Rais

Comments

comments