Makamu  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Tundu Lissu, ametuma salamu za Krismasi kwa Watanzania,akiwataka wanachama na wafuasi wa chama hicho kutokata tamaakatika jitihada zao alizoziita mapambano ya kudai haki.

Lissu ambaye amekuwa kimya tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu, kwa sasayuko Ubelgiji alikokwenda kutokana na kile alichodai sababu za usalama wake akihofu kuwapo watuwanaomfuatilia kwa malengo mabaya.

mtaalamu huyo wa sheria, ameahidi kuwa Januari Mosi, atatoa mwelekeo wa chama hicho namikakati mbalimbali kwa mwaka ujao.

Lissu aunguruma Ughaibuni

“Kwa wote hawa wenye njaa na kiu ya haki, ujumbe wangu wa Krismasi ni uleule alioueleza mwandishi wariwaya wa Kimarekani, Taylor Caldwell: “Hatuko peke yetu. Hata usiku unapokuwa wa giza zaidi, au upepo wabaridi kali, au ulimwengu unapoonekana kutokujali kabisa.”Hatuko peke yetu. Kwa hiyo tusivunjike moyo au kukata tamaa. Wiki ijayo, katika salamu zangu za MwakaMpya, nitazungumza kwa kirefu kidogo juu ya masuala haya na mengine na juu ya majukumu yetu kwa mwakaujao,” amesema  Lissu katika kipande cha video.

Lissu alishika nafasi ya pili katika Uchaguzi Mkuu uliopita nyuma ya Rais John Magufuli.

Kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo, mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki, alikuwa anaishi Ubelgji alikokwenda kwa ajili ya matibabu ya kibingwa baada ya kushambuliwa kwa risasi jijini Dodoma na watu wasiojulikana miaka mitatu iliyopita.

Magufuli azuia hoteli ya Sugu kubomolewa
Wawili wapoteza maisha kuporomoka kwa jengo la Beit Al Ajaib