Meneja wa klabu ya Man Utd, Louis van Gaal amekiri kufurahishwa na kasi ya kinda Marcus Rashford, ambaye jana aliiwezesha klabu hiyo kuchomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya mahasimu wao Man City.

Van Gaal, amesema kinda huyo anayecheza nafasi ya ushambuliaji, amekua na kasi ya kusaka mafanikio kwa haraka, tangu alipoanza kumtumia majuma kadhaa yaliyopita, hivyo ana imani atafika mbali.

Amesema inashangaza kwa kinda kama Rashford kuwa na kasi nzuri ya kujituma anapokua uwanjani na kufikia hatua ya kufunga mabao muhimu katika michezo ambayo imekua haidhaniwi kama ataweza kufunga.

Meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, amesisitiza kwamba kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, ataendelea kuwa sehemu ya mipango yake hadi mwishoni mwa msimu huu, ambapo anaamini watafanikiwa kufikia malengo.

Rashford aliifungia Man Utd bao la ushindi katika mchezo wa jana, daklika ya 16, ambalo lilitosha kuipa point tatu muhimu klabu hioyo ya Old Trafford ugenini.

Mpaka sasa Rashford ameshaifungia Man Utd mabao matano katika michezo minane aliyocheza, na bado anatabiriwa kufanya vizuri zaidi katika mapambano yaliyosalia kabla ya msimu wa 2015-16 haujafikia kikomo mwezi May.

Uchaguzi Zanzibar: Haya hapa matokeo ya majimbo kadhaa
Mwandishi wa DW aliyepotea apatikana