Leo Januari 9, 2018 aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Ngoyai Lowassa amemtembelea Ikulu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli na kufanya naye mazungumzo na kumpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya.

”Ameniomba mara nyingi nikutane nae na leo nimekutana nae, tumezungumza mambo mengi” amesema Magufuli.

Ambapo Lowassa ameshukuru kupata nafasi ya kuonana na Rais Magufuli, amekiri kwa kazi nzuri anayoifanya na kusema tuendelee kumtia moyo.

Aidha Lowassa ametaja maeneo ambayo Rais amefanya kazi kubwa inayoonekana kwa kila mtu.

“Moja na kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira,” Lowassa

“Stiegler’s Gorge ni kujenga ajira na mengine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira,  jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, kwa kweli nakushukuru  Rais, you made my day”  Lowassa.

Rais Magufuli amempongeza Edward Ngoyai Lowassa kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali na amesema Lowassa ni mmoja wa viongozi ambaye kwa wakati wake ametoa mchango katika nchi.

 

Mtuhumiwa bomba la mafuta ni mstaafu, Polisi watoa neno
Mtulia atii agizo la CCM