Kocha Mkuu wa Young Africans Luc Eymael amesema ataendelea kumpa nafasi mshambuliaji Yikpe Gnamien, kwa kuwa hana chaguo bora zaidi ya washambuliaji kwenye kikosi chake.

Mashabiki wa Young Africans wameonyesha dhahiri kutomkubali mshambuliaji huyo aliyefunga mabao mawili, moja kwenye ligi na jingine kwenye michuano ya Kombe La Shirikisho(ASFC) tangu aliposajiliwa mwezi Januari mwaka huu.

Mshambuliaji huyo utoka Ivory Coast anaonekana kuwa chaguo namba mbili kwenye safu ya ushambuliaji baada ya Ditram nchimbi ambaye ni chaguo la kwanza.

Yikpe anaonekana kuwapiku David Molinga na Tariq Seif ambao kwenye michezo ya karibuni wamekuwa na nafasi finyu kwenye kikosi cha kwanza

“Kwanza nataka mfahamu, sitaki kuzungumza mengi kuhusu Yikpe kwa kuwa sio mimi niliyemsajili, nilimkuta hapa”

“Lakini pia kwa sasa nalazimika kumtumia kwa sababu sina wachezaji zaidi kwenye safu ya ushambuliaji,” alisema Eymael

Inaelezwa Yikpe amekuwa akifanya vizuri mazoezini na hivyo kuwashawashi benchi la ufundi lakini amekuwa hafanyi vizuri anapopewa nafasi kwenye mechi.

Everiste Ndayishimye rais mpya Burundi, aapishwa
Hatma maombi ya kukamatwa Lissu Julai 14