Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ametoa onyo kali kwa vyama vya siasa nchini ambavyo vimetangaza kufanya mikutano ya hadhara kabla ya muda uliopangwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza kuwa, Jeshi la Polisi lipo imara hasa kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu mwakani, hivyo vyama vya siasa vilivyotangaza kuanza kampeni kabla ya muda Jeshi lake litavishughulikia ipasavyo.

Amesema kuwa Serikali ya Magufuli haiwezi kuchezewa na wanasiasa wanaotaka kuchafua amani ya nchi, hivyo wanaojaribu kumtikisa Rais Mafuguli hawatamuweza.

Aidha, Waziri Lugola, alipoulizwa kuhusu vituo vya polisi kutotoa dhamana saa 24 kama alivyoelekeza kwa nchi nzima, alishangazwa kama kuna baadhi ya vituo hivyo kuendelea kuvunja maagizo yake, hivyo ametoa namba yake ya simu ya mkononi na kuwataka wananchi kumpigia endapo watakuwa wanaonewa na askari yeyote wa idara yoyote anayoiongoza.

Hata hivyo, Waziri Lugola amepiga marufuku tabia ya Watanzania kuchukua sheria mkononi katika matukio yoyote yanayotokea nchini.

Japan yaonya kuhusu madeni ya nchi za Kiafrika
Kesi ya Erick Kabendera yaahirishwa tena