Mkuu wa Mkoa Mbeya, Albert Chalamila, amesema kuwa wananchi ambao walishambulia msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela Claudi Kitta, wamechagua kuuawa, kwa kile alichokieleza wao walionyesha nia ya kumuua Mkuu huyo wa Wilaya.

Ametoa kauli hiyo katika kata ya Ghana, jijini Mbeya ikiwa siku chache baada ya Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela kushambuliwa na wananchi wa Kijiji cha Mpunguti.

Amesema kuwa kwasababu walirusha mawe na walichagua kumuua Mkuu wa Wilaya ya Kyela na Kamati ya Ulinzi na Usalama, hivyo na wao wamechagua kuuawa.

”Hili nalisema sio kinyume cha haki za binadamu haki za binadamu walipaswa kuwa nayo wao, Nawaambieni ukweli hapa bado sijafungua kikosi kingine, tunasubiri watu waaanze tena ili tupige king’ora cha mwisho.” amesema Chalamila.

Mapema jana Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Jeromi Ngowi alisema kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini wale wote waliohusika na kuvamia msafara wa Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudi Kitta, katika Kijiji cha Mpunguti wilayani humo.

Kesi ya Erick Kabendera yaahirishwa tena
LIVE DAR ES SALAAM: Mkutano wa Wafanyabiashara wa mazao ya Nafaka JNICC