Maombi ya kupinga kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania, Airbus nchini Afrika Kusini yanatarajiwa kuanza kusikilizwa hii leo na mahakama kuu nchini humo.

Akizungumzia kesi hiyo, Wakili Mkuu wa Serikali msaidizi, Dkt. Ally Posi amesema kuwa mawakili kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa serikali kupitia ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali watashirikiana na mawakili wa serikali ya Afrika Kusini katika maombi ya kupinga kushikiliwa kwa Ndege hiyo.

”Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wanasimamia suala hilo, kuhakikisha Ndege hiyo inaachiwa,”amesema Dkt. Posi

Ndege hiyo ilishikiliwa kutokana na maombi namba 28/994/2019 yaliyowasilishwa na mwombaji, Hermanus Steyn kupitia ofisi ya uwakili ya Werksmans iliyopo nchini humo.

Aidha, maombi hayo ya kusikilizwa upande mmoja yaliwasilishwa Agosti 21 mwaka huu dhidi ya serikali ya Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Afrika Kusini.

Katika maombi hayo yaliambatanishwa na kiapo, kilichoapwa na Martin Richard Steyn na Bianka Pretorius wakisapoti maombi ya kuishikilia ndege hiyo kwasababu mdai anadai serikali ya Tanzania Dola za Marekani 36,375,672,81.

Mahakama ilisikiliza maombi hayo ya upande mmoja yaliyowasilishwa na mwombaji na kuamuru Ndege hiyo iwekwe kizuizini.

Mwaka 2010 mbele ya Jaji Mstaafu, Josephat Mackanja nchini humo, mdai alikuwa anadai fidia ya shamba lake jumla ya dola za Marekani milioni 36.

Hata hivyo, mahakama ilizitaka pande zote mbili wakaketi kwa ajili ya makubaliano ya Dola milioni 30.

Chanzo- Mtanzania

Video: Kigogo CCM akataa uteuzi, JPM, Mkapa, Mbeki waichambua Afrika
Mbwana Samatta kutikisa Ligi ya Mabingwa Ulaya