Meneja wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona Luis Enrique ameonyesha kuguswa na suala la kuumia kwa mshambuliaji wake kutoka nchini Argentina Lionel Messi ambaye atakua nje ya uwanja kwa majuma matatu.

Enrique amesema kuumia kwa Messi ni pigo kubwa kwa wadau wote wa soka duniani kutokana na mvuto alionao ndani na nje ya uwanja, hivyo kutokuwepo kwake kutasababisha mapungufu ya burudani.

Meneja huyo raia wa nchini Hispania, amedai kuwa pamoja na pigo hilo kuwa kwa wadau wote wa soka duniani, kwa upande wa FC Barcelona hakutokua na tabu kubwa kutokana na mipango aliyoiandaa ya kubadilisha mfumo ambao utakisaidia kikosi chake kucheza bila mshambuliaji huyo.

“Kutokuwepo kwa Lionel Messi ni pigo kwa wadau wote wa soka duniani, na kwa jambo hilo hatuna budi kuwaomba radhi,” Alisema Enrique. “Nitajitahidi kufanya kila linalowezekana ili kukiwezesha kikosi changu kucheza katika mfumo tofauti bila Messi.

“Ni kweli kutokuwepo kwa Messi huenda ikawa changamoto kubwa sana, lakini hakuna jambo ambalo halina mpango kazi namba mbili, hivyo tutahakikisha tunapambana na kufikia malengo ya kusaka point katika kila mchezo utakaotuhusu.” Aliongeza Enrique

Messi alipatwa na majeraha ya misuli ya paja akiwa katika mchezo wa ligi ya Hispania uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Atletico Madrid, na alishindwa kuendelea na mchezo katika dakika ya 56.

Mchezo huo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Camp Nou ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Mtego Wa Mauricio Pochettino Wamnasa Danny Rose
Marekani na Urusi zashambuliana vikali Umoja wa Mataifa