Uongozi wa Timu ya KMC FC umetangaza kumsimamisha mshambuliaji wake Realint Lusajo, aliyesajiliwa klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu akitokea kwa Wauaji wa Kusini Namungo FC.

Tarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya KMC FC Christina Mwagala imeelza kuwa, Lusajo amesimamishwa klabuni hapo kwa sababu za utovu wa nidhamu.

Christina amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya uongozi kujiridhisha kuwa mchezaji huyo alionesha utovu wa nidhamu, hivyo amelazimika kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni za KMC FC.

Amesema mchezaji  yoyote wa KMC FC anapofanya makosa ya utovu wa nidhamu kwenye timu anapaswa kupata adhabu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa.

Katika hatua nyingine Christina amesema uongozi wa KMC FC umetoa mapumziko ya siku 10 kwa wachezaji wake na kwamba watapaswa kurejea kambini Januari 15 mwaka huu kwa ajili ya kuanza maandalizi ya michezo ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara.

KMC FC wataendelea na Mshike Mshike wa Ligi hiyo inayoingia kwenye mzunguuko wa 19 kwa kucheza ugenini dhidi ya Tanzania Prisons.

Maalim Seif akemea ubaguzi wa rangi Zanzibar
Wanne wafariki baada ya wafuasi wa Trump kuvamia bunge