Maaskofu 34 wa Kanisa Katoliki nchini Chile wamemwandikia barua Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis kumuomba aridhie kujiuzulu kwao kutokana na kashfa ya udhalilishaji kingono iliyolikumba Kanisa hilo nchini humo.

Maaskofu hao wanatuhumiwa kwa kuzuia uchunguzi wa kashfa ya ngono inayomuhusu padre Fenando Karadima anayetuhumiwa kwa kumlawiti mtoto mdogo wa kiume.

Askofu Juan Barros ambaye anatuhumiwa kutumia wadhifa wake ndani ya Kanisa Katoliki kujaribu kuzuia uchunguzi dhidi ya tuhuma za udhalilishaji kingono zinazomkabili padre Fernando Karadima.

Maaskofu hao wameomba msamaha kwa waathirika na Kanisa kwa ujumla kwa makosa hayo makubwa na uzembe.

Aidha katika barua walioandika maaskofu hao wamesema maisha yao yapo mikononi mwa Papa na ikitokea hatokubaliana na ombi lao la kujiuzulu basi wataendelea kulitumikia kanisa na waumini wake.

Maaskofu hao wameamua kujiuzulu kama sehemu ya kutenda haki juu ya madhara waliosababisha kwa jamii na kanisa hivyo kulipa makosa yao wameamua kujizulu.

Watu mbalimbali walitoa maoni yao kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter wakimtaka Papa Francis akubaliane na ombi la jopo la maaskofu hao kujiuzulu.

Na mpaka sasa haijafahamika kama Papa Francis ameridhia ombi la Maaskofu hao kujiuzulu au lah.

 

Makonda apokea msaada wa Mamilioni ya ujenzi wa Ofisi za walimu Dar
Mwanafunzi afariki dunia jijini Mwanza