Mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani wameitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu wa Agosti 8, unafanywa kwa njia huru na ya haki

Katika misa maalum iliyoandaliwa na Kanisa la Kianglikana la All Saints na kuhudhuriwa na mamia ya Wakenya kutoka matabaka mbalimbali, mabalozi kutoka nchi za bara la Ulaya pamoja na Marekani wamelaani vikali mauaji ya kinyama ya mwishoni mwa wiki dhidi ya afisa mmoja wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC na wakaishinikiza serikali na vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa haraka.

“Ningependa kusema tu kwamba tunalaani mauaji hayo yaliyotokea kwa afisa wa tume ya uchaguzi kwani si jambo zuri hata kidogo na limeweka doa kwa nchi ya Kenya, Kuhusu uchunguzi huu tunaweza kuwa tayari kutoa msaada lakini kimsingi ni jukumu la Serikali ya Kenya kuamua jinsi inavyotaka kuendesha uchunguzi huo,” amesema Robert Godec, balozi wa Marekani nchini Kenya

Aidha, Marekani na Uingereza ni miongini mwa wafadhili wakubwa kutoka jumuiya ya kimataifa ambao wanatoa misaada ya aina mbali mbali kwa taifa nchini Kenya, ikiwemo miradi yenye lengo la kuimarisha demokrasia na utawala bora.

Hata hivyo, Kenya ipo katika kampeni za mwisho kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Agosti tarehe 8 mwaka huu ambapo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali baina ya mgombea wa chama cha Jubilee, Rais Uhuru Kenyatta anayegombea muhula wa pili dhidi ya mpinzani wake mkuu, Raila Odinga, mgombea wa muungano wa upinzani, NASA.

Ben Pol: Hakuna kilichotengenezwa ni maisha yangu halisi na Ebitoke
Jumba la professa J lapitiwa na bomoaboma, lapigwa X